Wakazi wa kijiji cha Kiruru Kata ya Lembeni Wilaya ya Mwanga - Kilimanjaro, wameanza kupata maji safi na salama kwa matumizi mbalimbali (matumizi ya nyumbani & mifugo).
Mradi huo ambao una
uwezo wa kuhudumia zaidi ya kaya 427 zenye wakazi zaidi ya 2,135 umejengwa na shirika la
Water Mission Tanzania, kwa ufadhili wa Rotary Club ya Mwanga & Rotary Club Seeside - USA,
Rotary International na Rotary Foundation.
Kata
ya Kiruru inayojumuisha vijiji vinne vya Heria, Msikitini, Bhughuru na Mighareni.
Uzinduzi wa mradi huu umefuatia tatizo la muda mrefu lililo kuwa likiwabili wananchi la ukosefu wa maji safi kutokana na kutokuwa na
vyanzo vya uhakika vya maji kutokana na mazingira ya kijiografia ya eneo hilo.
Mkuu
wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Aron Mbogho akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo. |
Mama Akitishwa Ndoo ya Maji na Mgeni Rasmi. |
Wataalam Ngazi ya Kata/Vijiji wa Kata ya Lembeni na Kijiji cha Kiruru na
Wananchi Wakiwa kwenye Sherehe za Uzinduzi.
No comments:
Post a Comment