Tuesday, 29 May 2018

Uzinduzi wa Mradi wa Maji - Kijiji cha Kiruru Mwanga (24/05/2018)


Wakazi wa kijiji cha Kiruru Kata ya Lembeni Wilaya ya Mwanga - Kilimanjaro, wameanza kupata maji safi na salama kwa matumizi mbalimbali (matumizi ya nyumbani & mifugo). 
Mradi huo ambao una uwezo wa kuhudumia zaidi ya kaya 427 zenye wakazi zaidi ya 2,135 umejengwa na shirika la Water Mission Tanzania, kwa ufadhili wa Rotary Club ya Mwanga & Rotary Club Seeside - USA, Rotary International na Rotary Foundation.
Kata ya Kiruru inayojumuisha vijiji vinne vya Heria, Msikitini, Bhughuru na Mighareni.

Uzinduzi wa mradi huu umefuatia tatizo la muda mrefu lililo kuwa likiwabili wananchi la ukosefu wa maji safi kutokana na kutokuwa na vyanzo vya uhakika vya maji kutokana na mazingira ya kijiografia ya eneo hilo.
Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mhe. Aron Mbogho akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa mradi huo.

Mama Akitishwa Ndoo ya Maji na Mgeni Rasmi.

Wataalam Ngazi ya Kata/Vijiji wa Kata ya Lembeni na Kijiji cha Kiruru na 
Wananchi Wakiwa kwenye Sherehe za Uzinduzi.

Check Alsohttps://www.ippmedia.com/en/business/2135-villagers-mwanga-district-get-access-clean-and-safe-water



Other Posts!

Official Mwanga

Welcome to Mwanga Rotary Club Blog Club President - S. Gasiano & Visitor from UK This blog will be used to post various ac...